Maswali
- Utaratibu wa kuchimba visima ukoje?
-
Ukitaka kuchimba kisima unatakiwa kufanya utafiti wa awali ili:-
- Kuangalia jiolojia ya eneo husika
- Kuangalia uwezekano wa kuwepo mikondo ya maji ardhini
- Historia ya eneo husika kuhusiana na suala la maji.
- Gharama za kuchimba kisima zikoje?
-
Gharama za kuchimba kisima/Visima hutegemea zaidi mambo yafuatayo:-
- Kipenyo na kina cha kisima pamoja na bomba zitakazotumika katika ujenzi.
- Aina ya mwamba utakaotakiwa kutobolewa.
- Umbali wa eneo la kuchimba kisima kutoka mahali ilipo mitambo yetu ya uchimbaji.
- Bei ya vifaa na mafuta (Dizeli) kwa wakati husika.
- Hali ya mazingira ya sehemu kitakapochimbwa kisima, mfano kama hakuna barabara, hivyo kuhitaji matengenezo ya njia ya kupitishia mitambo.
- Wingi wa vifaa vitakavyotakiwa kupelekwa eneo la uchimbaji kwa ajili ya shughuli hiyo mfano booster, compresor, mudpump, generator, welding plant, mobile workshop.
- Muda utakaotumika kupima uwezo wautoaji maji wa kisima husika.
- Kiasi na gharama za filtergravel, polymer bentonite, diesel, lubricants nk. vitakavyotumika katika uchimbaji.
- Gharama zote zinaweza kuandaliwa baada ya kupata ripoti ya utafiti wa eneo husika.
- Gharama za ujenzi wa bwawa zikoje?
-
Gharama za ujenzi wa bwawa unategemea mambo yafuatayo:-
- Uchunguzi wa mazingira.
- Upimaji wa ardhi (Topographical Survey).
- Utafiti wa udongo.
- Usanifu.
- Ripoti ya usanifu.
- Ujenzi wa bwawa.
- Kuna umuhimu gani wa kufanya utafiti kabla ya kuchimba kisima/Kujenga bwawa?
-
Faida za kufanya utafiti kabla ya kuchimba kisima/ kujenga bwawa ni kama ifuatavyo:-
- Inapunguza gharamza zisizokuwa za lazima kwa eneo litakaloonekana halifai kuchimba.
- Inapunguza hasara zitokanazo na visima visivyokuwa na maji ambavyo vilichimbwa bila kupimwa.
- Mteja hufahamu gharama halisi kabla ya kuanza mradi.
- Hupunguza gharama zisizokuwa za msingi kwa kuchimba kisima kirefu sababu kina cha kisima huongeza gharama.
- Mteja hupata kisiam/bwawa bora na kilichoondaliwa kitaalamu.