KM - MoW akikagua mitambo ya Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa
Posted on: July 19th, 2019Mkurugenzi Mkuu (DG) wa Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Gonsalves Rutakyamirwa akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo kuhusu aina na idadi ya mitambo inayotumika kuchimba visima na kujenga Mabwawa kote nchini na nje ya nchi. Tukio hili ilifanyika wakati Prof.Kitila Mkumbo alipotembelea Wakala kuangalia rasilimali vitu na kuongea na rasilimali watu waliopo wakati huu wa kipindi cha mpito.