Pata Kisima na Bwawa bora kwa gharama nafuu na kwa kujali thamani halisi ya pesa yako

Neno la ukaribisho

Kwa heshima, nakukaribisha rasmi kwenye tovuti ya Wakala wa Uchimbaji Visima na Ujenzi wa Mabwawa (DDCA). Lengo kuu la kuanzisha tovuti hii ni kuufanya Wakala kuwajibika na kuwa karibu na wadau wake na jamii kwa ujumla katika suala zima la kutekeleza majukumu yake ya kuwapatia wananchi vyanzo vipya vya maji kwa kuchimba visima, kukarabati na kujenga mabwawa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, mifugo, umwagiliaji, ufugaji wa samaki na viwandani.

Tovuti hii itapanua wigo mpana wa wadau kupata habari mbalimbali za DDCA kwa njia ya mtandao kama vile huduma na bidhaa mbalimbali zitolewazo na Wakala. Ni matumaini yetu kuwa wadau wetu na jamaii kwa ujumla wataitumia kikamilifu tovuti hii kwa faida. Tovuti hii inatupa mrejesho tunaoutarajia na sisi tupo tayari kushiriki katika kutoa taarifa wakati wowote zinapohitajika.